NGAO - MFUMO WA KUJILINGA
Nimfumo wa kujilinda wa Tanzania ulioanzishwa kwa lengo la kuwapatia raia uwezo wa kujilinda dhidi ya wanyang'anyi, wabakaji, wateka nyara, wauaji, magonjwa, na mazingira hatarishi na ajali. Mfumo huu u msanii na msanii wa sanaa za mapigano, issa rajabu tofiki, maaarufu kwa jina la "mlinzi shujaa" mwaka ( 2019 ) katika nchi ya tanzania. Mfumo wa ngao unamchanganyiko wa mafunzo imara na muhimu sana kwa kujilinda, ambayo imetoka katika karate, jujitsu ya Kijapani, kenpo ya kale, na kung fu.
MICHEZO YA OLIMPIKI
Hakuna kushiriki katika mashindano ya olimpiki kwa sababu, mafunzo yake ni kwa ajili ya kujilinda tuu, kwaiyo hata mbinu za ngoo zimepangiliwa kwa ya kushambulia na kulemaza au kuua kama ikibidi kwa muda mchche iwezekanavyo. Ngao ni mfumo wa kitili sana lakini unazingatia sana sheria ili kumlinda shujaa wa ngao asije kuimgia katika kesi za jinai.
ASILI YA NENO ( NGAO )
Ngao ni neno la kiswahili lenye asili ya kibaiolojia, ambalo maana yake kwa kifupi ni ( ( (silaha, ulinzi au ujuzi wa kujihami unaotumika kwa kuzuia madhara ya mashambulizi ya adui, au ni "ulinzi wa kuilinda nafsi, haki na mali " .
MBINU ZA NGAO
ngao hufundisha jinsi ya kusimama katika mapigano, mbinu za msingi za kurusha mikono na miguu, kukwepa, kutupa chini, kunyonga viungo , kabali nakadhalika. Pia ngao hufundisha jinsi ya kujitoa pindi utapo shikwa au kukumbatiwa au kukabwa kwa kabali, hufundisha jinsi ya silaha na silaha mwenye silaha ya kisu, upanga, nondo, kirungu, gongo la mti, chupa, mawe, nk,
MIKANDA YA MADARAJA
Katika mafunzo ya ngao - self defense hakuna madaraja ya mikanda ,bali kuna ngazi tatu tuu za mafunzo , ambazo ni junior, hii ni ngazi ya awali, senior hii ni ngazi ya kati, na ngazi ya mwisho kabisa ni master.
KUPIGANA
aina ya mashambulizi ya ngao, ngao wanashambulia kwa kasi kubwa, mapigo yao yanatoka kwa kasi sana kama nyoka anavyo shambulia. Pia, wanapiga katika maeneo dhaifu ambayo hayawezi kuimarika kwa mazoezi. Kama vile katika macho, pu, koo, nyuma ya shingo, ubavu wa shingo, chembe ya moyo, mbavu changa, spinal code, korodani, mikono na ugoko. Lengo kuu hapa nikumlemaza adui haraka iwezekana na kutoroka kurudi nyumbani salama.

Maoni
Chapisha Maoni